Michango kanisani : Gavana Lusaka atetea wanasiasa

Francis Ngala
1 Min Read
Gavana wa kaunti ya Bungoma Kenneth Lusaka ametetea viongozi wa Siasa wanaotoa michango kwa makanisa, akisema ishara kama hizo zinaendana na mafundisho ya Biblia.
Akizungumza hii leo wakati wa misa ya kutoa shukrani katika Kanisa la anglikana la mtakatifu Crispinus katika mji wa Bungoma, alikotoa mchango wa Shilingi Milioni 5 kutoka kwa Rais William Ruto, Lusaka alisisitiza kuwa kuunga mkono kazi ya Mungu ni jambo la kupongezwa.
Askofu wa Dayosisi hiyo ya Bungoma George Mechumo, ambaye aliongoza misa hiyo, aliunga mkono maoni ya Lusaka, huku akipuuzilia mbali ukosoaji dhidi ya michango ya kanisa, akisema michango kama hiyo ni muhimu kwa kuendeleza shughuli za kanisa.
Askofu huyo aliwakosoa viongozi wa makanisa wanaokubali shinikizo kutoka nje, akiwataka kuzingatia wajibu wao wa kiroho.
Askofu Mechumo alithibitisha kuwa dayosisi yake itaendelea kupokea michango kutoka kwa viongozi ilimradi itatumika kutimiza utume wa kanisa
Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.