Mgonjwa afariki katika hali tatanishi KNH

Tom Mathinji
1 Min Read
Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta.

Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH), imethibitisha kuwa mgonjwa aliyekuwa akipokea matibabu, amepatikana akiwa amefariki katika njia tatanishi, Alhamisi alasiri.

Kupitia ujumbe mfupi kwenye ukurasa wake wa X, Afisa Mkuu Mtendaji wa hospitali hiyo William Sigilai, mgonjwa huo alipataka amefariki muda mfupi baada ya saa nane mchana, wakati muda wa kuwatembelea wagonjwa ulipokamilika.

“Mnamo Julai 17,2025 saa nane mchana, punde tu baada ya muda wa kuwaona wagonjwa kukamilika,  mgonjwa alipatikana kwenye wadi ya wagonjwa akiwa ameloa damu. Mgonjwa huyo alifanyiwa uchunguzi na kubainishwa kuwa amefariki,” alisema Sigilai kupitia kwa taarifa hiyo.

Sigialai aliongeza kuwa hospitali hiyo imeripoti kisa hicho kwa Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai na asasi zingine za serikali, ili uchunguzi wa kifo hicho utekelezwe.

Kifo hicho kinajiri miezi miwili baada ya mgonjwa mwingine kupatikana akiwa ameariki huku akiwa na jeraha la kukatwa koo katika hospitali hiyo ya Kenyatta.

“Mawazo yetu yako na familia ya marehemu wakati huu mgumu wa majonzi,” ilisema taarifa hiyo.

TAGGED:
Share This Article