Waandalizi wa Makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japan, wamezindua medali zitakazoshindaniwa Septemba mwaka huu.
Medali hizo zilizinduliwa Alhamisi Juni 5 kuadhimisha siku 100 kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Kwa mara ya kwanza medali hizo zitachorwa majina ya washindi.
Tokyo,Japan itaandaa mashindano hayo kati ya Septemba 13 na 21 mwaka huu.