Mchuano wa mwisho ya kundi A kuwania kombe la CHAN kati ya Kenya na Zambia, Jumapili hii uwanjani Kasarani, umerejeshwa nyuma kutoka saa mbili usiku hadi saa tisa alasiri.
Mchuano huo utachezwa sambamba na ule kati ya DR Congo na Morocco katika uwanja wa Nyayo.
Hata hivyo, ni idadi ndogo ya mashabiki watakaofika uwanjani Kasarani baada ya CAF kupunguza idadi ya tiketi kutoka 48,000 hadi 27,000.
Kenya ni sharti waishinde Zambia ili kujihakikishia nafasi ya kwanza kundini humo na kuwa mwenyeji wa mechi ya robo fainali.