Mchina aliyemdhulumu raia wa Kenya afutwa kazi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa China aliyemdhulumu Mkenya, afutwa kazi.

Raia wa China aliyemdhulumu mkenya katika kiwanda cha TCM jijini Eldoret, amefutwa kazi. Hayo yamethibitishwa na ubalozi wa China nchini Kenya.

Kupitia kwa taarifa, ubalozi huo ulielezea kusikitishwa kwake na tukio hilo ambalo lilinaswa kwenye video iliyosambazwa kwa mitandao ya kijamii.

“Usimamizi wa kampuni hiyo umemsimamisha kazi mara moja raia huyo, na unakusudia kuchukua hatua zaidi za kinidhamu,” ulisema ubalozi huo.

Wakati huo huo ubalozi huo uliwahimiza raia wake wanaoishi na kufanya kazi hapa nchini kuzingatia sheria, kanuni na tamaduni za Kenya.

Ubalozi huo unasema unaamini kwamba tukio hilo la pekee halipaswi kuathiri ushirikiano wa uwekezaji kati ya kampuni za China na Kenya, lakini ni ukumbusho kwa raia wote wa China nchini Kenya kuzingatia kanuni ya kuheshimiana na marafiki wa Kenya na kuishi kulingana na sheria, kanuni, na mila za kitamaduni za Kenya.

TAGGED:
Share This Article