Mchekeshaji Mulamwah awapatia waandamanaji chakula

Tom Mathinji
1 Min Read
Mulamwa awapa waandamanaji chakula.

Mchekeshaji maarufu hapa nchini David Onyando almaarufu Mulamwah, amesifiwa na wafuasi wake mtandaoni kufuatia kitendo cha kuwalisha waandamaji jijini Nairobi.

Kwenye video aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, mcheshi huyo anaonekana akiwagawia waandamaji chai kwa mandazi.

Punde, idadi ya waandamanaji hao inaonekana ikiongezeka na kung’ang’ania chakula hicho, ishara tosha kuwa walikuwa wanakeketwa matumbo.

Hatua hiyo ya kuwapa waandamanaji chakula imeshabikiwa na wafuasi wake kama yenye utu kwa vijana wanaoandamana jijini na miji mingine nchini, ambao wanapinga mswada wa fedha wa mwaka 2024.

Wabunge 204 walipiga kura kuunga mkono mswada huo Alhamisi, huku wabunge 115 wakiupinga.

Mswada huo sasa utajadiliwa na kamati ya bunge lote, kabla ya kusomwa kwa mara ya tatu na kisha kupigiwa kura.

Vijana almaarufu Gen Z, walishiriki maandamano kote nchini, wakita mswada huo kutupiliwa mbali.

Share This Article