Harambee Stars ilisajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chad, katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki uliosakatwa jana usiku katika uwanja wa Marrakech nchini Morocco.
Emmanuel Osoro, aliyekuwa akivalia sare ya kwanza ya timu ya taifa, alipachika bao la kwanza kunako dakika ya 18 kabla ya David Sakwa kutanua uongozi muda mfupi kabla ya mapumziko.
Wenyeji ChadAki Mammar alikomboa bao hilo kunako dakika ya 60.
Ushindi huo ulikuwa wa kwanza kwa Kenya baada ya mechi sita tangu waibwage Tanzania mabao 2-1 uwanjani Gamboni.
Kenya na Chad walikuwa wametoka sare tasa katika mchuano wa kwanza wa kirafiki Jumamosi iliyopita.