Kocha Mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy, ametaja kikosi kwa mechi mbili za mwisho za kundi F, kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwezi ujao ugenini.
McCarthy amewaita kikosini wachezaji wawili kwa mara ya kwanza akiwemo beki anayesakata soka nchini Uingereza Vincent Harper na mshambulizi Lawrence Okoth wa timu ya chipukizi chini ya umri wa miaka 20.
Kenya itamenyana na Burundi tarehe 9 mwezi ujao mjini Bujumbura, kabla ya kufunga ratiba dhidi ya Ivory Coast siku 5 baadaye mjini Abidjan katika mechi za kundiF.
Harambee Stars ni ya tano katika kundi hilo kwa alama 9.
Kikosi hicho kitaraipoti kambini mapema mwezi ujao kabla ya kikosi cha mwisho kutajwa.
Kikosi
Makipa
Faruk Shikhalo, Byrne Omondi, Brian Bwire
Mabeki
Manzur Suleiman, Vincent Harper, Sylvester Owino, Alphonce Omija, Collins Sichenje, Michael Kibwage, Ronney Onyango, Abud Omar, Daniel Sakari
Viungo
Alpha Onyango, Duke Abuya, Timothy Ouma, Ben Stanley, Marvin Nabwire, Austine Odhiambo
Wingá
William Lenkupae, Job Ochieng, Boniface Muchiri
Washambulizi
Michael Olunga, Ryan Ogam, Lawrence Okoth