Mwakilishi Wadi (MCA) wa wadi ya Chwele Kabuchai, kaunti ya Bungoma James Barasa Mukhongo ameaga dunia.
Kifo chake kimetangazwa na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula.
“Ni kwa uchungu mkubwa na huzuni isiyofikirika kwamba natangaza kifo cha MCA wangu James Barasa Mukhongo wa wadi ya Chwele Kabuchai,” alisema Wetang’ula kwenye mtandao wake wa X leo Jumatatu.
Kulingana na Wetang’ula, hadi kifo chake, Mukhongo alikuwa amehudumu kwa kipindi cha mihula mitano.