Mahakama kuu ya Kampala nchini Uganda, imebatilisha matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa upinzani wa eneo bunge la Kawempe Kaskazini, Elias Luyimbaazi Nalukoola.
Mahakama kuu imeamrisha tume ya uchaguzi nchini humo kuandaa uchaguzi upya .
Kupitia kwa uamuzi uliotolea na jaji Bernard Namanya, kupitia kwa barua pepe, matokeo ya uchaguzi huo mdogo uliofanyika Machi 25 umefutiliwa mbali kwa kukiuka sharia za uchaguzi wa bunge.
Audidha Jaji Namanya amesema wapigaji kura 16,640, walizuiwa kupiga kura, akiwemo mwaniaji wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM), Nambi Farida Kigongo.
Kesi hiyo iliwasilishwa na Nambi aliyezoa kura 8,593, dhidi ya kura 17,764, alizopata Nalukoola na kutangazwa mshindi kwa tiketi ya chama cha National Unity Platform (NUP).