Maafisa wa Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC), wamemkamata mbunge wa Kajiado Magharibi George Sunkuyia, kwa madai ya kughushi vyeti vya masomo ya kidato cha nne (KCSE).
Kulingana na EACC, mbunge huyo atafunguliwa mashtaka ya kutoa habari za kupotosha na kuwasilisha cheti bandia.
“Mnamo Januari 30,2012 katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia (JKUAT) eneo la Juja, kaunti ya Kiambu, ukiwa na ufahamu uliwasilisha kwa msajili wa masomo katika chuo hicho cheti cha kidato cha nne chenye nambari za usajili 2988068, kikiwa na alama ya C+, ukisingizia kilikuwa halali kutoka kwa Baraza la Kitaifa la Mitihani,” ilisoma shtaka dhidi ya mbunge huyo.
Kwa sasa mbunge huyo anahojiwa na maafisa hao, kabla ya kufikishwa mahakamani.