Mbosso aahidi mashabiki wake kazi mpya hivi karibuni

Msanii huyo amesema kwamba kuna mambo anashughulikia kabla ya kuzindua miziki mipya.

Marion Bosire
1 Min Read

Miezi kadhaa baada yake kuondoka WCB, msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Mbosso ameahisi mashabiki zake kazi mpya hivi karibuni.

Mbosso alisema “Naona mashabiki zangu wakililia kazi mpya, niwaambie tu vilio vyao nimevisikia na navifanyia kazi, ila nimejipa muda kidogo wa kuweka baadhi ya mambo sawa.”

Msanii huyo alielezea kwamba kazi zipo na anaendelea kuandaa nyingine ambazo ataachilia katika muda usio mrefu akisema zitaondoa kiu ambayo mashabiki wako nayo.

Kando na kazi mpya za muziki msanii huyo amefafanua kwamba maisha yake hayajakuwa magumu kufuatia kuondoka kwenye kampuni ya muziki ya WCB.

Uvumi ulisambaa kwamba maisha yake yamebadilika pakubwa baada yake kuonekana nyumbani kwao huko Kibiti wengi wakidhania kwamba alirejea nyumbani kufuatia kufilisika.

Mbosso alisema anapenda mitandao lakini wakati mwingine yanayofanyika humo hayafurahishi. Alifafanua kwamba ana familia huko Kibiti na mambo mengine ambayo ni lazima ayashughulikie.

Mbosso aliondoka kampuni ya WCB inayomilikiwa na msanii mwenzake Diamond Platnumz mwezi Februari mwaka huu wa 2025 bila masharti yoyote kinyume na ilivyokuwa wakati wasanii wengine waliondoka humo.

Harmonize na Rayvanny walipoondoka WCB walilazimika kutoa malipo fulani kulingana na mikataba ambayo walitia saini wakiingia humo.

Share This Article