Mbivu na mbichi ya vipusa wa Kenya kubainika leo Tunis

Kenya ilifuzu kwa fainali za WAFCON kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets, itachuana na wenyeji Tunisia  leo katika mchuano wa marudio wa raundi ya kwanza kuwania kufuzu kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao WAFCON.

Pambano hilo litasakatwa mjini Tunis, huku mshindi akiweka miadi ya kumenyana na Gambia katika raundi ya pili.

Kocha wa Starlets Beldine Odemba, alisafiri na kikosi cha wanandinga 23 kwa mchuano wa leo, akilenga kurekebisha makosa ya waliyofanya wiki jana katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex, walipoambulia sarea tasa.

Vipusa wa Kenya wanalenga kuondoa nuksi ya kutoshinda mechi ugenini kwa miaka 19, ambapo wameshindwa mechi 10 mtawalia.

Kenya ilifuzu kwa fainali za WAFCON kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

Mshindi wa mechi ya raundi ya pili atajikatia tiketi kwa kipute cha mwakani cha WAFCON nchini Morocco.

 

 

 

Share This Article