Mauaji ya Were: Mahakama yafutilia mbali dhamana ya Philip Aroko

Tom Mathinji
1 Min Read
Mfanyabiashara Philip Aroko.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), imefanikiwa kukata rufaa ya kuachiliwa kwa mfanyabiashara Philip Aroko.

Aroko alikamatwa tena baada ya mahakama kuu ya Kibera kubatilisha hatua ya kumwachilia kwa dhamana.

Aroko alikamatwa mnamo Jumatatu jioni baada ya kuachiliwa kwa dhamana Ijumaa iliyopita kusubiri matokeo ya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya aliyekuwa mbunge wa Kasipul Charles Were.

Aroko aliachiliwa siku ya Ijumaa kwa dhama ya shilingi 300,000 na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Irene Gichobi.

Hakimu huyo alitoa masharti kadhaa ya kuachiliwa kwa Aroko ikiwa ni pamoja akabidhi mamlaka hati yake ya kusafiri, kuripoti kwa afisi za DCI mara mbili kwa wiki na kuhakikisha anapatikana anapohitajika.

Aroko na washukiwa wengine, walikamatwa kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya mbunge wa Kasipul marehemu Charles Were.

TAGGED:
Share This Article