Matokeo ya tathmini ya KJSEA kutangazwa tarehe 11 Disemba

Tom Mathinji
1 Min Read
Matokeo ya tathmini ya KJSEA kutangazwa Disemba 11,2025.

Matokeo ya tathmini ya gredi ya 9 KJSEA, yatatangazwa Disemba 11, 2025, huku shughuli ya kuteua shule watakazojiunga nazo ikitarajiwa kuanza wiki moja baadaye.

Katibu wa Elimu ya Msingi Prof. Julius Bitok, amesema barua za kujiunga na shule zitatolewa kabla ya siku kuu ya Krismasi, na kwamba wanafunzi wote milioni 1.1 wanatarajiwa kuanza masomo ya Sekondary Msingi Januari 12, 2025.

Prof. Bitok alihakikisha kuwa uhamisho kutoka shule ya junia sekondari hadi shule ya senior sekondari utakuwa mzuri, na akaongeza kuwa sera ya serikali kuhusu elimu ya msingi bila malipo na elimu ya sekondari bila malipo haijabadilika, akipuuza uvumi kwamba serikali inapanga kusitisha ufadhili wa shule.

Katibu Bitok alisisiriza kwamba mitihani ya kitaifa ya mwaka huu imekuwa yenye uaminifu kwa kiasi kikubwa licha ya kuwa na watahiniwa milioni 3.4.

Share This Article