Masud Juma kukosa mechi ya Angola kesho

Kulingana na Kocha mkuu wa Kenya Benni McCarthy, mshambulizi huyo alijeruhiwa akiwa mazoezini na hawezi hatarisha kumjumuisha kikosini dhidi ya Angola.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mshambulizi wa timu ya taifa Harambee Stars Masud Juma atakosa mchuano wa kesho wa kundi A kuwania kombe la CHAN kati ya Kenya na Angola kutokana na jeraha.

Kulingana na kocha mkuu wa Kenya Benni McCarthy, mshambulizi huyo alijeruhiwa akiwa mazoezini na hawezi hatarisha kumjumuisha kikosini dhidi ya Angola.

“Masud alikuwa na mchango mkubwa kwenye mechi yetu dhidi ya DRC, lakini baada ya kupata jeraha, itabidi tujipange. Tunatumai atarejea kwa mechi zijazo,” alisema McCarthy.

Harambee Stars itakabiliana na Angola kesho kuanzia saa moja usiku katika uwanja wa Kasarani wakihitaji ushindi kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali.

Share This Article