Masomo yatatizika Algeria kufuatia mgomo wa Walimu

Dismas Otuke
1 Min Read

Mgomo wa kitaifa wa walimu nchini Algeria, umeingia siku ya pili leo huku walimu wakilalamika kuhusu kulipwa mishahara midogo na mazingira duni ya kazi.

Shughuli za masomo zilitatizika jana huku wanafunzi wakisalia nje ya madarasa baada ya walimu kukosa kufika shuleni.

Walimu wengi waliohitimu nchini humo wamekuwa wakihamia mataifa ya kigeni kutafuta ajira.

Licha ya Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune kuongeza mishahara ya wafanyikazi wa umma kwa asilimia 37 katika muhula wake wa kwanza, bado walimu wanadai kubaguliwa kwa mazingira mabovu.

 

Share This Article