Mashujaa 142 kutuzwa mwaka huu

Tom Mathinji
1 Min Read

Mashujaa 142 kutoka pembe zote za taifa, watatuzwa wakati wa sherehe za Mashujaa za mwaka huu, zitakazoandaliwa katika kaunti ya Kwale.

Kamishna wa eneo la Pwani Rhoda Onyancha amesema Mashujaa 22 kati yao wanatoka katika eneo la Pwani.

“Mashujaa 142 tayari wamefika hapa Kwale kutuzwa. Ni vyema wageni hawa wajihisi kuwa wanatambulika,” alisema Onyancha.

Kulingana na mrakibu huyo wa Pwani, milango ya Uwanja wa Kwale itafunguliwa saa kumi alfajiri, huku akitoa wito kwa wakazi wa eneo hilo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria sherehe hizo

Wakati huo huo Onyancha alisifu kuandaliwa kwa sherehe za Kitaifa katika kaunti tofauti, akisema hatua hiyo imepiga jeki chumi za kaunti husika, Kwale ikiwemo.

Katika kaunti ya Kwale, Onyancha alisema sherehe hizi zimesababisha kuimarishwa kwa miundo mbinu, mfano mwema ukiwa kupanuliwa kwa Uwanja wa ndege wa Diani ambao unatarajiwa kuongeza idadi ya wageni wanaozuru kaunti hii.

“Kupanuliwa kwa Uwanja wa ndege wa Diani, kutasababisha ongezeko la wageni wanaozuru kaunti ya Kwale na maeneo yaliyo karibu,” alisema Onyancha.

Share This Article