Mashirika ya serikali yanajizatiti kupata namba mpya za usajili wa magari kabla ya kukamilika kwa muda uliowekwa na Mkuu wa Utumishi wa umma Felix Koskei.
Kupitia kwa ilani iliyochapishwa Mei 21,2025, Koskei aliagiza kuwa magari yote ya serikali ni sharti yawe na namba mpya za usajili wa magari kufiki Agosti 29, 2025.
Magari ambayo hayatakuwa na nambari hizo mpya, yatakamatwa kwenye msako wa kitaifa utakaotekelezwa na Halmashauri ya Uchukuzi na Usalama Barabarani (NTSA) kitengo cha ukaguzi ww magari ya serikali (GVCU).
Koskei alisema, nambari hizo mpya za usajili zilizoanzishwa miaka miwili iliyopita, zinaafikia viwango vya kimataifa.
Kulingana na Koskei, namba hizo za kisasa za usajili wa magari zinalenga kukabiliana na visa vya wizi wa magari.