Mashemeji Derby kupigwa Homa Bay, Juni 2

AFC Leopards na Gor waliambulia sare tasa katika mkumbo wa kwanza uliopigwa uwanjani Nyayo Machi 30 mwaka huu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wanaoondoka wa Ligi kuu ya Kenya Gor Mahia wametangaza kuandaa derby ya mashemeji dhidi ya watani wao AFC Leopards Jumatatu ijayo Juni 2 katika uwanja wa Raila Odinga kaunti ya Homa Bay.

AFC Leopards na Gor waliambulia sare tasa katika mkumbo wa kwanza uliopigwa uwanjani Nyayo Machi 30 mwaka huu.

Mechi hiyo ya raundi ya 33 hata hivyo haitakuwa na uzito kwani  Gor, ambao wana  uwezo finyu wa kutwaa ubingwa wa ligi Kuu wakihitaji kushinda mechi zote tatu na kutarajia Police FC, watapoteza mechi zao mbili za mwisho ili wahifadhi taji.

Gor watafunga msimu na Police  FC Juni 15.

Mechi hiyo iliahirishwa awali kutokana na kukosa kwa uwanja.

 

 

Share This Article