Marupurupu ya wanagenzi wauguzi na matabibu yapunguzwa

Tume ya kuratibu mishahara ilitangaza mwezi Machi kuwa wanagenzi watakuwa wakipokea marupuruou yasiyozidi shilingi 25, 000 kwa mwezi.

Dismas Otuke
1 Min Read
Mary Muthoni - Katibu katika Wizara ya Afya

Marupurupu ya wauguzi wanagenzi na matabibu yamepunguzwa kufuatia agizo la mahakama wiki jana.

Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni amesema kuwa wanagenzi wapya watakaoajiriwa watapokea marupurupu yaliyopunguzwa jinsi ilivyoamrishwa na mahakama.

Wanagenzi wapya wa shahada watakuwa wakipokea marupurupu ya kati ya shilingi 27,000 na 35,000, wakati wanagenzi wa utabibu wakipokea kati ya shilingi 47,000 na 70,000.

Wanagenzi Wafamaisa watalipwa kati ya shilingi 47,000 na 70,000.

Serikali kwa sasa imewaajiri matabi wanagenzi 145 wa sahada 1,270 wa stashahada ya utabibu na wauguzi wanagenzi wa stashahada 1,283.

Tume ya kuratibu mishahara ilitangaza mwezi Machi kuwa wanagenzi watakuwa wakipokea marupuruou yasiyozidi shilingi 25 ,000 kwa mwezi.

Share This Article