Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, umetoa tahadhari ya kiusalama kwa raia wake wanaoishi nchini humo, kufuatia wito wa maandamano unaotarajiwa kuandaliwa Disemba 9, 2025.
Kulingana na ubalozi huo, shughuli za maandamano nchini Tanzania huenda zikaanza mapema, huku ikiwataka raia wa Marekani kuchukua tahadhari na kudokeza uwezekano wa machafuko, mari ya kuto-toka nje, ukosefu wa intaneti, matatizo ya uchukuzi wa Feri kuelekea Zanzibar, kuahirishwa kwa safari za ndege za kimataifa na vizuizi vya barabarani.
Aidha ubalozi huo umesema kuwa raia wa kigeni wanafanyiwa uchunguzi hasaa ikiwa wanamiliki vifaa vya kielekroniki, kubainisha iwapo wanauhusiano wowote na ghasia au nakala zozote za kisiasa.
“Polisi wamewakumbusha raia kuwa chini ya sheria za nchi hiyo usambazaji picha au video zinazoweza sababisha taharuki ni hatia ya kiuhalifu,” ulisema ubalozo huo.
Ubalozi huo umewahimiza raia wa Marekani kujiepusha na ghasia, umati wa watu, kuweka hifadhi ya kutosha ya maji na chakula, dawa na pesa taslimu iwapo itahitajika.