Marekani imeapa kuwapokonya Viza wanafunzi wa Uchina wanaosomea Marekani, wakiwemo wale walio na uhusiano wa karibu na chama cha kikomunisti au wanaosomea taaluma mahususi.
Waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani Marco Rubio alitangaza haya jana .
Mamia ya maelfu ya wanafunzi wa Uchina wanaosomea nchini Marekani, wataathiriwa na agizo hilo jipya hatua ambayo pia itaathiri vibaya vyuo vya marekani vinayotegemea karo ya wanafunzi.
Rubio ameongeza kuwa watafanya ukaguzi wa kina wa maombi ya viza ikiwemo ya kutoka Uchina na Hong Kong.