Marehemu Ong’ondo Were kuzikwa leo Kasipul

Mwendazake, mbunge huyo, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana tarehe 30 mwezi jana katika barabara ya Ngong.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were ,aliyeuawa kwa kupigwa risasi mwishoni mwa mwezijana, atazikwa leo nyumbani kwake Kachien, Kaborok kaunti ya Homa Bay.

Mwili wa marehemu Were, uliwasilishwa jana mjini Oyugis, huku maelfu ya waombolezaji wakijitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa mbunge huyo wa chama cha ODM.

Gavana wa kaunti hiyo, Gladys Wanga,jana aliongoza msafara wa magari yaliyosindikiza mwili wa marehemu kutoka uwanja mdogo wa Kabunde hadi nyumbani kwake.

Waombolezaji walitazama mwili katika shule ya msingi ya Agoro Sare, punde baada ya kuwasilishwa jana jioni.

Viongozi wakuu serikalini na wanasiasa wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo.

Mwendazake, mbunge huyo, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana tarehe 30 mwezi jana katika barabara ya Ngong.

Tayari polisi wamewatia mbaroni washukiwa 9 wakiwemo dereva na mlinzi wake, kuhusiana na mauaji hayo ya kinyama.

Share This Article