Marefa watakaosimamia kipute cha CHAN

Dismas Otuke
3 Min Read

Zikiwa zimesalia wiki mbili kabla ya kipute cha mashindano ya CHAN 2024 kung’oa nanga, Shirikisho la soka barani Afrika CAF, limetangaza orodha ya waamuzi 70 watakaochezesha michuano hiyo.

Katika orodha hiyo, kuna waamuzi wa kati 26, waamuzi wasaidizi 26 na waamuzi wa VAR 18, ambapo bendera ya Kenya, itawakilishwa na waamuzi watatu tu; Nyagrowa Dickens Mimisa, Mwangi Samuel Kuria na Stephen Yiembe.

Mimisa atakuwa miongoni mwa waamuzi wa 26, Kuria akiungana na waamuzi wengine wasaidizi 25 huku Yiembe yeye akiwa miongoni mwa waamuzi wa 18 walioteuliwa kusimamia VAR (Video Match Officials).

Makala haya ya nane yataandaliwa na mataifa matatu ya Kenya, Uganda na Tanzania, kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano hayo, kuanzia Agosti 2-30.

Hii hapa ni Orodha kamili ya marefa wa CHAN 2024:

WAAMUZI WA KATI

Radissa Abdoul Raphiou Ligali (Benin), Messie Jessie Oved Nvoulou (Congo), Kpan Clement Franklin (Côte d’Ivoire), Malala Kabanga Yannick (DR Congo), Ahmed Nagy Mosa Mahmoud (Egypt), Tsegay Teklu Mogos (Eritrea), Jammeh Lamin N. (Gambia), Nyagrowa Dickens Mimisa (Kenya).

Ahmed Abdulrazg (Libya), Diakhate Ousmane (Mali), Milazare Patrice (Mauritius), Loutfi Bekouassa (Algeria), Diouf Adalbert (Senegal), Jelly Chavani (South Africa), Ahmed Arajiga (Tanzania), Aklesso Gnama (Togo), Melki Mehrez (Tunisia), Lucky Razake Kasalirwe (Uganda)Vincent Kabore (Burkina Faso), Brahamou Sadou Ali (Niger), Brighton Chimene (Zimbabwe), Mefire Abdou Abdel (Cameroon), Bouchra Karboubi (Morocco), Shamirah Nabadda (Uganda), Kech Chaf Mustapha (Morocco) na Houssam Benyahya (Algeria).

WAAMUZI WASAIDIZI
Ngila Guilain Bongele (DR Congo), Lucky Kegalogetswe (Botswana), Sanou Habib Judicael Oumar (Burkina Faso), Emery Niyongabo (Burundi), Rodrigue Menye Mpele (Cameroon), Amaldine Soulaimane (Comoros)
Alao Salim (Benin), Fasika Biru Yehualashet (Ethiopia), Jawo Abdul Aziz (Gambia), Addy Roland Nii Dodoo (Ghana), Mwangi Samuel Kuria (Kenya), Joel Wonka Doe (Liberia), Nassiri Hamza (Morocco), Yacouba Abdoul Aziz (Niger)
Dieudonne Mutuyimana (Rwanda), Omer Hamid Mohammed Ahmed (Sudan), Wael Hanachi (Tunisia), Ronald Katenya (Uganda), Eleyeh Robleh (Djibouti), Ettien Eba Medard (Côte d’Ivoire), Abeigne Ndong Amos (Gabon)
Wengine ni, Sirak Samuel (Eritrea) Ally Hamdani Said (Tanzania), Malondi Chany (Congo), Adel Abane (Algeria) na Diana Chikotesha wa Zambia.

WAAMUZI WA VIDEO (VAR)
Mahmoud Ashour (Egypt), Dahane Beida (Mauritania), Lahlou Benbraham (Algeria), Bamlak Tessema Weyesa (Ethiopia), Samir Guezzaz (Morocco), Hamza El Fariq (Morocco), Issa Sy (Senegal), Atcho Prierre Ghislain (Gabon), Daniel Lareya (Ghana)Abongile Tom (South Africa), Yasir Abdalaziz (Sudan), Viana Letticia (Eswatini), Maria Rivet (Mauritius), Akhona Makalima (South Africa), Stephen Yiembe (Kenya), Atezambong Fomo Carine (Cameroon), Jermoumi Fatiha (Morocco), na Ghorbal Mustapha kutoka Algeria.

 

 

TAGGED:
Share This Article