Marafiki wa mwigizaji nyota wa Marekani Bryshere Gray wamesema kwamba anachohitaji ni usaidizi na ushauri nasaha na wala sio kifungo gerezani.
Wazo hili ni la Dustin “Chosen” Wilkins ambaye pia ni mwigizaji na mwanamuziki na ambaye aliwasilisha kesi mahakamani dhidi ya Bryshere mwezi Juni baada yao kuzozana katika hoteli moja ya Virginia.
Dustin anasema alichukua hatua ya kuwasilisha kesi hiyo kwa sababu Gray anaugua maradhi ya akili ambayo yanazidi kuwa mabaya kutokana na hatua yake ya kukoma kutumia dawa zake na anatumia pombe.
Anahisi kesi hiyo itamfanya Gray arejelee matibabu.
Dustin ambaye alikuwa anajiandaa kushirikiana na Gray kwenye kipindi cha matukio halisi cha “The Starboy” kabla yao kuzozana hotelini, anamtetea rafiki yake akisema huwa anawajibika sana kwa kutumia dawa zake na hujichunga asizidishe kiwango cha pombe.
Hata hivyo Chosen anahisi kwamba Bryshere hutengwa kwa urahisi na watu ambao hawamjali. Anamtaja mwigizaji huyo ambaye alifahamu hivi maajuzi kwamba ameachwa na kampuni yake ya mahusiano, kuwa kakake mdogo.
Hiyo ndiyo sababu anamjali sana na anajali kitakachomtokea kufuatia kesi aliyowasilisha dhidi yake.
Chosen yuko tayari kuondoa kesi hiyo mahakamani iwapo Bryshere ataahidi kujitolea kufuatilia kwa makini matibabu yake ya afya ya akili na kuangazia usalama wake.
Dustin “Chosen” Wilkins aliwasilisha kesi hiyo dhidi ya Bryshere Juni 13, 2025 na kibali cha kumkamata kikatolewa na akakamatwa Juni 15, 2025.
Bryshere anatarajiwa kufika mahakamani mwisho wa mwezi huu.