Hafla ya maombi ya kitaifa yaliyoratibiwa kuandaliwa Alhamisi Mei 29, yamerejeshwa nyuma hadi Jumatano tarehe 28 mwezi huu.
Maombi hayo yanaandaliwa na bunge la kitaifa na yatafanyika katika mkahawa wa Safari Park Hotel.
Hafla hiyo imekuwa ikiandaliwa kila Alhamisi ya mwisho ya mwezi Mei.
Maombi hayo huudhuriwa na viongozi wa matabaka mbalimbali huku Rais William Ruto pia akitarajiwa kuhudhuria.