Mamia ya wakazi wa Kikambala wanufaika kwa matibabu ya bure ya macho

Watu zaidi ya 30 walifanyiwa upasuaji wa macho kuondoa uvimbe katika kambi hiyo ya matibabu iliyofadhiliwa na kampuni ya Pwani Oil.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamia ya wakazi wa kijiji cha Kikambala, kaunti ya Kilifi, walinufaika kwa msaada wa kambi ya bure ya matibabu ya macho.

Watu zaidi ya 30 walifanyiwa upasuaji wa macho kuondoa uvimbe katika kambi hiyo ya matibabu iliyofadhiliwa na kampuni ya Pwani Oil.

“Lengo letu ni kuwa jamii zilizo na afya bora na nguvu na siyo kuwatibu magonjwa pekee bali pia kuwawezesha na kuwapa hadhi,” alisema Mkurugenzi wa biashara katika kampuni ya Pwani Oil.

Wakazi zaidi ya 340 walifanyiwa uchunguzi wa macho kwenye kambi hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na kituo cha afya cha Lions.

Share This Article