Sudan almaarufu Nile Crocodiles, iliwachabanga Super Eagles kutoka Nigeria magoli 4-0 ,katika mchuano wa kundi D kuwania kombe la CHAN .
Mechi hiyo iliyochezwa kiwarani Amaan mjini Zanzibar ilishuhudia Leonard Ngenge wa Nigeria akijipiga bao dakika ya 25 na kuwapa Sudan uongozi kabla ya Walieldin Khidir kuongeza la pili mwishoni mwa kipindi cha kwanza.
Abdelrazig Omer alitikisa nyavu mara mbili kunako kipindi cha pili na kuwachupisha Sudan uongozini mwa kundi D kwa alama 4 sawa na Senegal waliolazimisha sare ya bao moja dhidi ya Congo.
Nigeria ilikuwa timu ya kwanza kuyaaga mashindano baada ya kupoteza mechi ya pili.