Mama Rachel azuru Marakwet ,atoa msaada kwa manusura

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkewe Rais Rachel Ruto siku ya Jumamosi  amezuru eneo la Chesongoch, Marakwet Mashariki lililoathiriwa na maporomoko ya ardhi wiki moja iliyopita.

Mama taifa alizuru eneo la maporomoko hayo na baadaye kuwatembelea manusura waliolazwa hospitalini na kisha kutoa msaada wa chakula, mavazi na malazi kwa waathiriwa walio kambini.

Bi Ruto aliandamana na mawaziri Kipchumba Murkomen wa Usalama wa Taifa, Davis Chirchir wa Uchukuzi ,na maafisa wengine wakuu serikalini.

Zaidi ya watu 30 walifariki kwenye mkasa huo.

Share This Article