Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara, John Heche, amesafirishwa hadi Tarime na Jeshi la Polisi baada ya kukamatwa leo asubuhi.
Gaston Garubindi, wakili mkurugenzi wa Sheria wa Chama cha CHADEMA, amethibitisha hilo na kusema “Mheshimiwa Heche alipokuja mahakamani asubuhi alikamatwa na jeshi la Polisi kwa makosa ambayo hawajasema…”.
Jambo la John Heche halipo Dar es Salaam bali lipo Tarime na kuwa tayari ameshasafirishwa kuelekea huko, kulingana na Wakili Gaston.
Wakili Gaston aliongeza kuwa kama chama wanajipanga kwa ajili ya mawakili waliopo mkoa wa Mara na wengine kutoka Mwanza kwa ajili ya kutoa huduma za kisheria.
Akizungumza leo asubuhi, Katibu Mkuu alisema makamu mwenyekiti hakuwa amepewa wito wowote wakuitwa.
Heche alikamatwa akiwa njiani kuelekea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu.