Maafisa wa Polisi wamewanasa majambazi waili waliokuwa wamemteka nyara afisa wa shirika la wanyamapori nchini KWS mtaani Kinoo kaunti ya Kiambu mapema Jumatatu.
Yamkini polisi walianza kulifuata gari lilikuwa na majambazi hao waliomteka nyara afisa wa KWS mapema Jumatatu na wakajaribu kuhepa walipolifumaniwa.
Wawili kati ya majambazi hao walitiwa mbaroni huku afisa wa KWS, akipatikana akiwa amefungwa mikono na miguu kwa kamba nyuma ya gari hilo.
Mwathiriwa huyo alikiri kuibiwa pesa na simu ya rununu na kudai kuwa majangili hao walikuwa wakisimamisha magari barabarani na kuwapora wasafiri waliokuwa wakielekea Nairobi.
Polisi walipata simu za rununu kutoka kwa majambazi hao huku wengine waliotoroka wakiwasakwa.