Majambazi sita wanaswa na polisi Mbooni

Dismas Otuke
1 Min Read

Washukiwa sita Wa ujambazi katika barabara kuu ya Mbumbuni, kaunti ndogo ya Mbooni mashariki walitiwa nguvuni na maafisa wa polisi Jana.

Hii inafuatia malalamishi yaliyowasilishwa mwendeshai gari mmoja kwenye barabara hiyo ambaye aliibiwa kimabavu Na henge.

Sita hao waliokamatwa ni Richard Muthoka, Mwenda Mutuku, Alex Musembi, James Musembi, Kevin Kioko, na Dennizs Mambo.

Majambazi hao ambao walipatikana Na bidhaa za wizi pia walipatikana na bunduki na wako korokoroni wakisubiri kufikishwa kortini.

TAGGED:
Share This Article