Mahakama yaamrisha kubomolewa kwa daraja la Pangani ndani ya miezi mitatu

Serikali imetakiwa kubomoa daraja hilo ndani ya siku 90 zijazo kwa kukiuka sheria.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetakiwa kubomoa kivuko cha abiria kilicho katika eneo la Pangani katika barabara kuu ya Thika, kwa kujengwa katika ardhi ya kibinafsi bila kumlipa mmiliki wa kipande hicho cha ardhi.

Jopo linaloshughulikia kesi za umiliki wa ardhi nchini limesema kuwa sehemu ya daraja hilo ambalo huwa ni kivuko kwa wawanaotembea kwa miguu lilijengwa katika ardhi ya kibinafsi.

Serikali imetakiwa kubomoa daraja hilo ndani ya siku 90 zijazo kwa kukiuka sheria.

Share This Article