Mahakama Kuu nchini Uganda imeahirisha kutoa hukumu juu ya ombi la kupewa dhamana kwa Dkt. Kizza Besigye mwanasiasa mkongwe wa upinzani aliyekamatwa mwaka uliopita nchini Kenya.
Uamuzi wa iwapo Besigye angepewa dhamana ulitarajiwa kutolewa leo lakini umeahirishwa hadi Desemba tarehe 29.
Mwanasiasa huyo anakabiliwa na mashataka ya uhaini pamoja na msaidizi wake wa kisiasa Hajji Obeid Lutale na afisa mmoja wa jeshi Dennis Ola.
Bado hawajakiri au kukanusha mashtaka hayo. Dkt Besigye na Lutale walikamatwa mwezi Novemba mwaka uliopita wakiwa mjini Nairobi nchini Kenya.