Mahakama: KBC ni mmiliki halali wa ardhi ya Komarock

Tom Mathinji
1 Min Read
Mahakama yaamua kwamba KBC ndiye mmiliki halali wa ardhi ya Komarock.

Shirika la utangazaji nchini KBC, limepata ushindi mahakamani kwenye kesi ya muda mrefu ya mzozo wa ardhi.

Hii inajiri baada ya mahakama ya kusikiza kesi za ardhi na kimazingira katika kaunti ya Machakos kuamua kwamba shirika la KBC, ndio mmliki wa shamba la takriban hekta 500 katika eneo la Komarock, kaunti ya Machakos ambako kuna kituo cha mitambo ya upeperushaji matangazo.

Kwenye uamuzi uliotolewa leo , mahakama hiyo ilisema ardhi hiyo ilio kwenye barabara ya Kangundo , ilitwaliwa na serikali kwa minajili ya utangazaji na kwamba chama cha umiliki ardhi cha Komarock kilipewa fidia .

Mahakama hiyo iliamua kwamba KBC inamiliki ardhi hiyo kwa niaba ya serikali ya Kenya. Mahakama hiyo pia ilitoa agizo la kutogawanywa kwa ardhi hiyo, kuuzwa pamoja na kutozwa kwa faini ya shilingi milioni moja kwa yeyote atakayeingia kwenye ardhi hiyo bila idhini.

Uamuzi huo unatamatisha kesi hiyo iliyowasilishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2013, ambako shirika la utangazaji nchini KBC , lililalamikika kuhusu kugawanywa kwa shamba hilo na kutishia shughuli za utangazaji za shirika hili.

TAGGED:
Share This Article