Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, aliwapokea mabingwa wa Ulaya Paris Saint Germain kwenye Ikulu siku ya Jumapili, baada ya kuwasili kutoka Ujerumani .
Macron alikashifu vurumai iliyozuka jijini Paris, punde baada ya kipinga cha mwisho cha fainali hiyo na zaidi ya mashabiki 600, wakikamatwa na polisi huku magari zaidi ya 20 yakiteketezwa.
Wachezaji na mashabiki walisherehekea ushindi huo mepema Jumamosi jijini Paris walipopiga gwaride .
PSG waliichabanga Inter Milan mabao 5-0, na kunyakua kombe la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza.