Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuwa mabwanyenye wanaotaka uraia wa Marekani watalazimika kulipia dola bilioni tano sawa na shilingi bilioni 650 za Kenya.
Kwenye taarifa hiyo, Trump amesema matajiri hao watalipia Gold Card, ambayo itachukua mahali pa Green Card ya sasa, ambayo huwawezesha wawekezaji wa kigeni kuishi na kufanya kazi Marekani na hatimaye kupewa uraia wa kudumu.
Marekani itaanzisha mpango huo katika kipindi cha majuma mawili yajayo.