Wachimba madini katika kijiji cha Hellu, eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit, wamepata mabomu 23 yaliyokuwa yamefukiwa chini ya ardhi.
Kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo, alithibitisha kupatikana kwa mabomu hayo, huku akiwahimiza wakazi wa eneo hilo kusitisha shughuli zote za uchimbaji madini katika eneo hilo.
Kulingana na afisa huyo mkuu wa polisi, mabomu hayo yaliyopatikana siku ya Jumamosi, ni ya ukubwa kwa milimita 81 kila moja.
Kimaiyo aliongeza kuwa kitengo cha maafisa wa kutegua mabomu cha Vikosi vya Ulinzi hapa nchini KDF, kimetumwa katika eneo hilo.
Mabomu hayo yanaaminika yaliachwa katika eneo hilo, nyakati za utawala wa wakoloni