Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Mpira wa Wavu kwa Wanaume, General Service Unit, na Kenya Ports Authority, waliomaliza nafasi ya pili msimu jana, wamegutushwa baada ya kuambulia kichapo siku ya Jumapili katika ukumbi wa uwanja wa Ksarani katika mechi za ligi kuu.
GSU walipigwa dafrau seti 3-0 za 25-21, 25-13, na 25-22 na timu ya Polisi wa Uwanja wa Ndege (KAPU).
Kenya Ports Authority (KPA) waliomaliza wa pili msimu jana walipigwa na butwaa waliposhindwa seti 2-3 na limbukeni Eldowas iliyopandishwa ngazi msimu huu kwa seti za 25-19, 27-29, 26-28, 25-11, 11-15.
Kwenye matokeo mengine, Magereza waliibwaga Prisons Nairobi seti 3-0 (25-21, 25-22, 25-23) huku Equity Bank pia ikipata ushindi wa seti 3-1 dhidi ya Rift Valley Prisons (25-17, 17-25, 25-21, na 25-13).