Maandamano ya kupinga serikali kuendelea Ijumaa nchini Togo

Gnassingbe aliye na umri wa miaka 86 amekuwa Rais wa Togo tangu mwaka 2005

Dismas Otuke
1 Min Read

Maandamano yanaarajiwa kuendelea nchini Togo leo Ijumaa, kupinga hatua ya serikali kutekeleza katiba mpya ambayo ilimruhusu Rais wa muda mrefu Faure Gnassingbé kusalia mamlakani katika wadhfa wa Waziri Mkuu.

Takriban waandamanaji watano wameangamia tangu kuanza kwa maandamano hayo majuma kadhaa yaliyopita kwenye makabiliano baina ya raia na polisi mjini Lome.

Katiba mpya iliyopitishwa nchini Togo mwaka jana bila kufanyiwa kura ya maoni ilibuni kiti cha Waziri Mkuu ambaye ana mamlaka makuu huku mamlaka ya Rais yakipunguzwa.

Gnassingbe aliye na umri wa miaka 86 amekuwa Rais wa Togo tangu mwaka 2005,alitwaa hatamu za kuwa Waziri mkuu   mwezi Mei mwaka  huu ,huku Jean-Lucien Savi de Tové, akichaguliwa na wabunge kuwa Rais.

Wadadisi wengi wanahoji hatua hiyo ya Gnassingbé, wakisema anataka kusalia mamlakani kwa muda mrefu zaidi kinyume cha sheria.

Share This Article