Maafisa wawili wa zamani wa NCPB washtakiwa kwa uhalifu wa kiuchumi

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wawili wa zamani wa NCPB washtakiwa kwa uhalifu wa kiuchumi.

Mahakama ya kukabiliana na ufisadi ya Milimani, imewapata maafisa wawili wa zamani wa Halmashaur ya Nafaka na Mazao (NCPB), mwanabiashara na kampuni mbili na makosa ya uhalifu wa kiuchumi.

Kulingana na mahakama hiyo, washukiwa hao wanatuhumiwa kwa kuuza mbolea ya ubora wa kiwango cha chini ya thamani ya shilingi milioni 209.

Washukiwa hao ni pamoja na Joseph Kiplangat Ngetich, John Mbaya Matiri, mwanabiashara Josiah Kariuki Kimani, kampuni ya  Fifty-One Capitals Limited na SBL Innovate Manufacturers.

Mahakama hiyo ilifahamishwa kuwa stakabadhi ghushi zilitumika kuihadaa shirika la ukadiriaji ubora wa bidhaa (KEBS).

Hata hivyo mahakama hiyo ilimwondolea lawama aliyekuwa Mkurigenzi Mkuu wa NCPB  Joseph Muna Kimote, kwa ukosefu wa ushahidi.

Kesi hiyo itatajwa Oktoba16, 2025.

TAGGED:
Share This Article