Maafisa wawili wa KDF wafunguliwa mashtaka ya mauaji

Tom Mathinji
1 Min Read

Washukiwa wawili wanaohusishwa na mauaji ya kikatili ya Mercy Rufani mwenye umri wa miaka 26, wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo Alhamisi.

Joseph Ngera Kamau na Fred Mathenge Kanja, ambao ni maafisa wa vikosi vya ulinzi nchini KDF, wametajwa kwa wa mwisho kuonekana na Mercy, ambaye mwili wake ulipatikana umetupwa katika mtaa wa Mwiki, Jijini Nairobi.

Baada ya uchunguzi wa kisayansi, maafisa wa upelelezi waliwafumania washukiwa hao katika mtaa wa Komarock na Tononoka mtawalia.

Kwa sasa wawili hao wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kasarani.

Mercy aliripotiwa kutoweka Septemba 28,2024 kutoka nyumbani kwa wazazi wake, katika mtaa wa Pipeline, Embakasi, Jijini Nairobi.

Kulingana na idara ya upelelezi wa makosa ya Jinai, Joseph Ngera alimchukua Mercy na kumbeba kwa gari aina ya  Mazda yenye nambari za usajili KDA 796L, na kumpeleka nyumbani kwake katika mtaa wa Komarock.

DCI iliripoti kuwa mzozo uliibuka baina ya wawili hao na Kamau anadaiwa kumgonga Mercy hadi kufa. Kamau alimpigia simu Kanja aje amsaidie kuutupa mwili wa Mercy.

TAGGED:
Share This Article