Maafisa wa NACADA waliopewa habari za kijasusi kutoka kwa umma wakishirikiana na polisi walifumania bangi hiyo iliyopakiwa ndani ya magunia 12 iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea Nairobi.
Mshukiwa mkuu wa Nancy Atieno Otieno, pia alinaswa wakati wa msako huo na kupelekwa katika korokoro ya Kisumu akisubiri kufikishwa mahakamani.
Afisa Mkuu mtendaji wa NACADA Dkt. Anthony Omerikwa amewapongeza wananchi kwa kushirikiana katika vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati.