Maafisa 2 wa zamani wa polisi wahukumiwa miaka 35 jela kila mmoja

Martin Mwanje
0 Min Read

Mahakama Kuu imewahukumu maafisa wawili wa zamani wa polisi kifungo cha miaka 35 jela kila mmoja. 

Maafisa waliohukumiwa kifungo hicho ni Emmanuel Barasa na Godwine Wekesa.

Hii ni baada ya mahakama kuwapata wawili hao na hatia ya kumuua Dennis Lusava katika kituo cha polisi cha Likuyani katika kaunti ya Kakamega.

Inasemekana maafisa hao walimtesa Lusava hadi akafariki na kisha kuutupa mwili wake katika Mto Nzoia.

Share This Article