Maafikiano kumi kati ya UDA na ODM

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) na Orange Democratic Movement (ODM) vimebuni ushirikiano wa kisiasa katika hafla iliyoandaliwa katika Ukumbi wa KICC.

Vyama hivyo viwili vimeafikiana kushirikiana katika masuala kumi kuu yafuatayo:

1. Utekelezaji kikamilifu wa ripoti ya uwiano wa kitaifa maarufu kama NADCO

2. Usawa katika ugavi wa Pato la Taifa (GDP) na nyadhfa za uongozi

3. Kulinda na kuimarisha ugatuzi

4. Uwekezaji wa kiuchumi kwa vijana

5. Kuleta uadilifu na uongozi bora

6. Kudumisha uhuru wa kujumuika na kulipa dhamana kwa kesi zote za wanaharakati

7. Kufanya ukaguzi wa hesabu kuhusu deni la serikali na jinsi pesa hizo zilivyotumika

8. Kupambana na ufisadi

9. Kuzuia matumizi mabaya ya rasilimali za serikali

10. Kulinda uhuru wa wananchi, kuzuia utekaji nyara, kuheshimu sheria, na uhuru wa raia

Ushirikiano huo umeashiria muungano mpya wa kisiasa na unapiga jeki azma ya Rais William Ruto kutetea wadhifa wake wakati wa uchaguzi mkuu ujao.

Hafla hiyo ya leo Ijumaa ilihudhuriwa na maafisa wote wakuu serikalini na wanasiasa kutoka kwa vyama vyote viwili.

Share This Article