Sherehe za kuadhimisha miaka 20 tangu kubuniwa kwa chama cha Orange Democratic Movement (ODM), zilizoanza Ijumaa Novemba 14, zitakamilika leo katika kaunti ya Mombasa.
Siku ya kwanza ya sherehe hizi ilikuwa na hisia kali wanachama wakitoa heshima na kumkumbuka mwanzilishi wa chama hayati Raila Odinga, aliyefariki mwezi uliopita.
Wanachama walilumbana vikali huku baadhi Yao wakiwashutumu wenzao Kwa kukinadi chama Kwa maslahi ya kibifsi..
Gavana wa Siaya James Orengo aliapa kuwa kamwe chama hicho hakitamuunga mkono Rais William Ruto, bali kitajisimamia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027.
Pia Mbunge wa EALA ambaye ni bintiye hayati Raila Winnie Odinga, alisema kamwe hawatakubali chama hicho kubuni muungano bali kitaendeleza harakati za Odinga za kupigania haki za wanyonge.