Kundi la waasi wa M23 limeripotiwa kuwateka nyara wagonjwa 130 wanaume kutoka kwa hospitali mbili mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki iliyopita.
Kwa mjibu wa ripoti kutoka Umoja wa Mataifa UN, M23 walivamia hospitali CBCA Ndosho na Heal Africa, Ijumaa iliyopita, na kuwateka nyara wanaume 130, 116, na 15 kutoka kwa kila hospitali mtawalia.
Wanaume hao wanakisiwa kuwa wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.
Zaidi ya watu 7,000 wameauwa mjini Goma tangu Januari mwaka huu kufuatia mapigano kati ya wanjeshi wa serikali ya Congo na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda.