Maafisa kutoka Kitengo cha Ulinzi wa Miundombinu Muhimu CIPU) wamenasa lori linaloshukiwa kusafirisha chuma za reli zilizoibwa katika eneo la Kibini.
Maafisa hao walinasa lori hilo kwa ushirikiano na maafisa wenzao kutoka kituo cha polisi cha Sultan Hamud baada ya kudokezewa na umma juu ya usafirishaji huo.
Baada ya lori hilo lenye nambari ya usajili KDL 139H kufanyiwa ukaguzi katika kituo cha polisi cha Sultan Hamud, lilipatikana likiwa limebeba slipa 61 za reli na nguzo 60 za reli zinazoshukiwa kuondolewa kwenye reli.

Mshukiwa aliwekwa kizuizini na lori kuzuiwa huku uchunguzi zaidi ukiendelea kabla ya kufikishwa mahakamani.