Liverpool kutotumia tena jezi nambari 20 kwa heshima ya marehemu Jota

Jota alifariki na kakake mdogo André Silva, kwenye  ajali ya barabarani Julai 4 mwaka huu akiwa Uhispania kuelekea Uingereza.

Dismas Otuke
1 Min Read

Usimamizi wa klabu ya Liverpool umetangaza kutotumia tena jezi nambari 20, iliyokuwa ikivaliwa na marehemu mshambulizi Diogo Jota.

Jota aliyekuwa na umri wa miaka 28, alitua ugani Anfield mwaka 2020 akitokea Wolves na kuwasaidia kushinda kombe la Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya 20 msimu uliopita.

Liverpool imesema haitakuwa inatumia tena jezi hiyo kwa timu zake zote kama njia ya kumheshimu Jota.

Jota alifariki na kakake mdogo André Silva, kwenye ajali ya barabarani Julai 4 mwaka huu akiwa Uhispania kuelekea Uingereza.

Share This Article